Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton
BIG 4 MILL BY FESTO ERNESTY,
Johannesburg. Siku chache kabla ya kusherehekea
siku yake ya kuzaliwa, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,
Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton, amemtumia salamu maalumu za
kumtakia sherehe njema.
Clinton ambaye ni rafiki wa karibu na familia ya
Mandela, aliyeungana na Dalai Lama na Askofu wa nchi hiyo, Desmond
Tutu, walituma salamu kwa njia ya video kwa vyombo vya habari jana.
Julai 18, Mandela anatarajiwa kutimiza miaka 95.
Mandela, ambaye alilazwa hospitali ya magonjwa ya
moyo tangu Juni 8 mwaka huu, anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu. Hata
hivyo, hali inatajwa kuwa siyo mbaya wala nzuri.
Maelfu ya Waafrika Kusini wamekuwa wakiomba usiku na mchana kuomba walau afikie miaka 95.
Hali hiyo inajionyesha hasa kutokana na watu wengi kufika hospitalini kumtakia kheri, licha ya hali yake kuwa mbaya.
“Ni taharuki tu hapa, sioni kama kuna hali ya kawaida,” alisema Irene Lambert, Mwalimu mwanafunzi kutoka Johannesburg.
Mwalimu huyo na mpenzi wake, walifika hospitalini
hapo wakiwa na picha ya Mandela na kadi yenye ujumbe kwake na kusema:
“Tumekuja na ujumbe huu kwa ajili ya Mandela, lakini tutawapa familia
kwa kuwa yeye hawezi kuusoma.”