BIG 4 MILL

big4mill.blogspot.com.

Usisite kutembelea blog yako

Karibu nawe mahali popote... - big4mill.blogspot.com.

Tunaishi pamoja wakati wowote

http://www.big4mill.blogspot.com for more info - big4mill.blogspot.com.

Kazi zetu ni...

Tunaelimisha, kuburudisha na kadhalka.

Pata habari mbalimbali

Ndani na nje ya Tanzania/ kitaifa na Kimataifa - big4mill.blogspot.com.

Saturday, 8 June 2013

  huko nchini china hari bado tete harakati za ukombozi bado ngumu

 
 
[image: Shughuli za uokozi baada ya tetemeko] Shirika la habari la taifa la Uchina linasema kuwa watu 150 wamekufa katika tetemeko kubwa la ardhi ambalo limeporomosha majengo na bara-bara katika jimbo la Sichuan, kusini-magharibi mwa nchi. Wanajeshi kama 6000 wamepelekwa kwenda kusaidia katika uokozi zaidi ya kilomita 100 kutoka Chengdu, mji mkuu wa jimbo la Sichuan . Shughuli za uokozi zinatatanishwa na bara-bara zilizovunjika na simu zilizokatika. Waziri Mkuu, Li Keqiang, aliwasili huko haraka kuongoza shughuli hizo. Tetemeko lilotokea katika jimbo la Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa w... more »

changa moto za mziki za mchaganya"ally nipishe


 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Nipishe amesema kuwa tasnia ya muziki kwa msanii chipukizi ina changamoto nyingi ambazo humkwamisha katika kuyafikia mafanikio kwa uharaka zaidi.
Akizungumza na Starehe, Nipishe aliyeanza muziki mwaka 2005, alisema ilimchukua muda mrefu kuyafikia mafanikio kimuziki, kutokana na changamoto nyingi zilizokuwa zikimkwamisha hasa kiuchumi.
“Niliwahi kutembea kwa miguu kutoka nyumbani Manseze kwenda studio iliyokuwepo eneo la Biafra lililopo Kinondoni B, na tulipohami Ukonga Wilaya ya Ilala, nilitembea kutoka huko hadi Biafra, wakati mwingine nilipatwa na masaibu njiani na nilipofika studio niliambiwa nirudi siku nyingine, wakati huo nikiwa na ari kubwa ya kufanya kazi,” alisema Nipishe.
Ali Nipishe anayetamba na wimbo ‘My’ anasema licha ya changamoto hizi wasanii wanapaswa kutumia nguvu kubwa na akili, kuwekeza kile kidogo wanachokipata kupitia kazi zao za kimuziki.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Kili Music Awards 2013 leo! Kitimtim MLIMANI CITYVANESSA MDEE

VANNESA MDEE



Hatimaye siku imetimia, ile siku ambayo kila mja na muungwana katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya alikuwa akiingoja, usiku wa tunzo za Kilimanjaro Tanzania, zitaunguruma kuanzia saa moja hadi kuendelea, Watanzania takriban 32 wanaofanya kazi katika tasnia ya muziki wanatarajiwa kuondoka na tunzo mikononi mwao leo.
Zaidi ya wasanii 100 wametajwa kuwania tunzo hizi, na wote wana imani ya ushindi na watakuwa ukumbini leo pamoja na baadhi ya mashabiki wao, kushuhudia matokeo ya kazi ngumu waliyoifanya katika msimu uliopita wa muziki wa Tanzania.
Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, kilichodhamiria kupeleka muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio, leo ndiyo mwenyeji wa shughuli husika na wameahidi usiku wa kihistoria, huku wakiadhimisha mwaka wa 13, wa tunzo hizi ambazo kila kukicha zinazidi kujizolea umaarufu.
George Kavishe, ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro na amefanya mahojiano na gazeti hili kuhusiana na usiku wa leo na mambo muhimu makubwa matatu yametajwa katika kuunogesha usiku mwingine wa tunzo, uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu
Kwanza, usiku hautakuwa Dar es Salaam peke yake utakuwa katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro na Dar ambapo katika viwanja mbalimbali vya Taifa Dar es Salaam, Mabatini Mwanza, na CCM Mkoa kwa Kilimanjaro kutakuwa na TV kubwa zitakazokuwa zikionyesha moja kwa moja tukio la utoaji tunzo litakalokuwa likiendelea katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa leo.
................................................................................................................................................................

My Blog List