Saturday, 8 June 2013

changa moto za mziki za mchaganya"ally nipishe


 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Nipishe amesema kuwa tasnia ya muziki kwa msanii chipukizi ina changamoto nyingi ambazo humkwamisha katika kuyafikia mafanikio kwa uharaka zaidi.
Akizungumza na Starehe, Nipishe aliyeanza muziki mwaka 2005, alisema ilimchukua muda mrefu kuyafikia mafanikio kimuziki, kutokana na changamoto nyingi zilizokuwa zikimkwamisha hasa kiuchumi.
“Niliwahi kutembea kwa miguu kutoka nyumbani Manseze kwenda studio iliyokuwepo eneo la Biafra lililopo Kinondoni B, na tulipohami Ukonga Wilaya ya Ilala, nilitembea kutoka huko hadi Biafra, wakati mwingine nilipatwa na masaibu njiani na nilipofika studio niliambiwa nirudi siku nyingine, wakati huo nikiwa na ari kubwa ya kufanya kazi,” alisema Nipishe.
Ali Nipishe anayetamba na wimbo ‘My’ anasema licha ya changamoto hizi wasanii wanapaswa kutumia nguvu kubwa na akili, kuwekeza kile kidogo wanachokipata kupitia kazi zao za kimuziki.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
,
“Kwa sasa ninapata shoo mbalimbali ambazo zinaniingizia fedha. Ninajitahidi kuwekeza huku na kule ili angalau niweze kuyamudu maisha kwa siku zijazo,” alisema bila kufafanua.
Nipishe alianza muziki mwaka 2005 na ilipofika mwaka 2007 alijiunga na Nyumba ya Vipaji (THT-Tanzania House of Talent), mbako yupo hadi sasa. Akiwa THT amefanikiwa kufanya kazi kadhaa ikiwamo wimbo wa ‘Tanzania Go’, Mapito alioshirikishwa na Mwasiti Almas na ‘My’ alioutoa mwaka 2013
.
Alisoma katika shule ya msingi LA Kisosora iliyopo jijini Tanga, baada ya kumaliza alijiunga katika kundi la muziki lililojulikana kama Hard Boys.

0 comments:

Post a Comment

My Blog List