BIG 4 MILL

big4mill.blogspot.com.

Usisite kutembelea blog yako

Karibu nawe mahali popote... - big4mill.blogspot.com.

Tunaishi pamoja wakati wowote

http://www.big4mill.blogspot.com for more info - big4mill.blogspot.com.

Kazi zetu ni...

Tunaelimisha, kuburudisha na kadhalka.

Pata habari mbalimbali

Ndani na nje ya Tanzania/ kitaifa na Kimataifa - big4mill.blogspot.com.

Wednesday, 10 July 2013

Clinton amtumia Mandela heri ya kuzaliwa

Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton
BIG 4 MILL BY FESTO ERNESTY,
Johannesburg. Siku chache kabla ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton, amemtumia salamu maalumu za kumtakia sherehe njema.
Clinton ambaye ni rafiki wa karibu na familia ya Mandela,  aliyeungana na Dalai Lama na Askofu wa nchi hiyo, Desmond Tutu, walituma  salamu kwa njia ya video kwa vyombo vya habari jana. Julai 18, Mandela anatarajiwa kutimiza miaka 95.
 Mandela, ambaye alilazwa hospitali ya magonjwa ya moyo tangu Juni 8 mwaka huu, anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu. Hata hivyo,  hali inatajwa kuwa siyo mbaya wala nzuri.
Maelfu ya Waafrika Kusini wamekuwa wakiomba usiku na mchana kuomba walau afikie miaka 95. 
Hali hiyo inajionyesha hasa kutokana na watu wengi kufika hospitalini kumtakia kheri, licha ya hali yake kuwa  mbaya.
“Ni taharuki tu hapa, sioni kama kuna hali ya kawaida,” alisema Irene Lambert, Mwalimu mwanafunzi kutoka Johannesburg.
Mwalimu huyo na mpenzi wake, walifika hospitalini hapo wakiwa na picha ya Mandela na kadi yenye ujumbe kwake na kusema: “Tumekuja na ujumbe huu kwa ajili ya Mandela, lakini tutawapa familia kwa kuwa yeye hawezi kuusoma.”

Kenya yaongoza kwa ufisadi


Yaongoza kwa ufisadi kati ya nchi 107 ambako utafiti huo ulifanyika,jambo ambalo limewasikitisha waken

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Transparency International, Kenya imeshika nafasi ya nne kwa ufisadi ikiwa ni  miongoni mwa nchi 107 ambako utafiti huo ulifanyw.
Ripoti hiyo ilibaini kwamba Wakenya saba kati ya 10 waliohojiwa walisema wamewahi kutoa hongo maishani mwao ili waweze kupata huduma moja hadi nane kati ya zilizochunguzwa.
Kulingana na utafiti huo, maofisa wa polisi ndio waliopatikana kuwa mafisadi zaidi nchini wakifuatiwa na wabunge, vyama vya kisiasa, mahakama na wafanyakazi wa Serikali.
Wakenya wengi walisema vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kidini hazina ufisadi mwingi.
Nchi fisadi zaidi duniani ni Sierra Leone ambako asilimia 84 ya watu waliohojiwa walikubali kwamba wametoa hongo. Sierra Leone inafuatwa na Liberia (asilimia 75) na Yemen (asilimia 74).
Nchi ambazo zilipatikana kuwa na ufisadi finyu ni Finland, Japan, Australia, Denmark, Uhispania, Canada, Ureno, Uruguay, Norway, New Zealand, Korea Kusini na Malaysia ambako watu zaidi ya 95 kati ya 100 waliohojiwa walisema hawajaona ufisadi wowote nchini mwao.
Katika eneo la Afrika Mashariki, Kenya ndiyo nchi fisadi zaidi ikifuatwa na Uganda (asilimia 61) na Tanzania (asilimia 56). Kulingana na utafiti huo ambao watu 114,000 walihojiwa, Rwanda ilipatikana kuwa na ufisadi mdogo zaidi katika eneo la Afrika Mashariki. Raia 13 pekee kati ya 100 wa nchi hiyo walikubali mwamba wametoa hongo. Ufisadi ulipatikana kukithiri zaidi barani Afrika. Baadhi ya nchi fisadi zaidi Afrika ni Zimbabwe, Msumbiji, Libya na Cameroon (zote zikiwa na asilimia 62) na Nigeria (asilimia 44).

Mghana alivyouawa kinyama Bagamoyo

 
Mbali na Marwa, ambaye amesoma kozi ya urubani, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Peter Charles Mayalla, ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo

Dar es Salaam. Salimu Mohamed Marwa (25) ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa magari, raia wa Ghana, Jose ph Opong.
Mbali na Marwa, ambaye amesoma kozi ya urubani, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Peter Charles Mayalla, ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo.
Washtakiwa hawa hao, ambao wote ni wakazi wa Bagamoyo mkoani Pwani wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, inayosikilizwa na Jaji Njengafibili Mwaikugile.
Wanadaiwa kuwa Septemba 10, 2010, walimuua kwa makusudi Opong, kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili, baada ya kumlewesha kwa dawa za kulevya na kisha kwenda kumzika katika msitu wa Kaole.
Awali Marwa, alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, baada kukamatwa akiwa na nyaraka za magari ya marehemu Opong katika harakati za kuyauza magari hayo yaliyokuwa Bandarini.
Alikamatwa baada ya mke wa marehemu Opong kutoa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi, Septemba 22, kuwa mumewe alikuwa hajaonekana tangu Septemba 9, na kwamba aliondoka kwenda kushughulikia magari yake yaliyokuwa bandarini.
Baada ya taarifa hizo, Polisi walitoa taarifa bandarini kuwa mtu yeyote atakayefika kutaka kutoa magari hayo asiruhusiwe, na Septemba 28, ndipo Salim alipokamatwa akiwa na nyaraka za magari hayo, mkataba wa mauziano na kitambulisho cha marehemu Opong.
Kwanza alipoulizwa kuhusu mahali alipozipata nyaraka hizo alisema kuwa ameuziwa na Joseph Opong, lakini alipoulizwa mahali alikokuwa Opong alijibu kuwa hajui na kwamba baada ya kuuziana, waliachana.
Kuhusu kitambulisho ambacho kilikuwa na jina la Opong lakini kikiwa na picha yake, alishindwa kueleza lolote.
Hivyo kesho yake Septemba 29, timu ya Upelelezi kutoka Polisi Kanda ya Dar es Salaam ikiongozwa na Inspekta (Mkaguzi wa Polisi), Saidi Mohamed Mwagara ilikwenda na mtuhumiwa nyumbani kwake Bagamoyo, kufanya ukaguzi ambao ungewezesha kubaini alikokuwa Opong.
Inspekta Mwagara alidai kuwa hata hivyo katika ukaguzi wao hawakuweza kupata kielelezo chochote cha kuwasaidia, na kwamba wakati wakiwa kwa mtuhumiwa huyo, alimtaka mtuhumiwa awaeleze ukweli kwa kuwa walikuwa wameshachoka
.
Alidai kuwa mshtakiwa huyo alisema naye ameshachoka kuzunguka na kwamba sasa anataka awaeleze ukweli, na ndipo akasema kuwa Opong tayari wameshamuua, na kwamba yuko tayari kwenda kuwaonyesha walikomzika.

My Blog List