Mbali na Marwa, ambaye amesoma kozi ya urubani, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Peter Charles Mayalla, ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo
Dar es Salaam. Salimu Mohamed Marwa (25) ni mshtakiwa wa kwanza
katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa magari, raia wa Ghana, Jose
ph Opong.
Mbali na Marwa, ambaye amesoma kozi ya urubani,
mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Peter Charles Mayalla, ambaye ni
mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo.
Washtakiwa hawa hao, ambao wote ni wakazi wa
Bagamoyo mkoani Pwani wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, inayosikilizwa na Jaji Njengafibili Mwaikugile.
Wanadaiwa kuwa Septemba 10, 2010, walimuua kwa
makusudi Opong, kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili, baada ya
kumlewesha kwa dawa za kulevya na kisha kwenda kumzika katika msitu wa
Kaole.
Awali Marwa, alitiwa mbaroni kwa tuhuma za
kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, baada kukamatwa akiwa na
nyaraka za magari ya marehemu Opong katika harakati za kuyauza magari
hayo yaliyokuwa Bandarini.
Alikamatwa baada ya mke wa marehemu Opong kutoa
taarifa Kituo Kikuu cha Polisi, Septemba 22, kuwa mumewe alikuwa
hajaonekana tangu Septemba 9, na kwamba aliondoka kwenda kushughulikia
magari yake yaliyokuwa bandarini.
Baada ya taarifa hizo, Polisi walitoa taarifa
bandarini kuwa mtu yeyote atakayefika kutaka kutoa magari hayo
asiruhusiwe, na Septemba 28, ndipo Salim alipokamatwa akiwa na nyaraka
za magari hayo, mkataba wa mauziano na kitambulisho cha marehemu Opong.
Kwanza alipoulizwa kuhusu mahali alipozipata
nyaraka hizo alisema kuwa ameuziwa na Joseph Opong, lakini alipoulizwa
mahali alikokuwa Opong alijibu kuwa hajui na kwamba baada ya kuuziana,
waliachana.
Kuhusu kitambulisho ambacho kilikuwa na jina la Opong lakini kikiwa na picha yake, alishindwa kueleza lolote.
Hivyo kesho yake Septemba 29, timu ya Upelelezi
kutoka Polisi Kanda ya Dar es Salaam ikiongozwa na Inspekta (Mkaguzi wa
Polisi), Saidi Mohamed Mwagara ilikwenda na mtuhumiwa nyumbani kwake
Bagamoyo, kufanya ukaguzi ambao ungewezesha kubaini alikokuwa Opong.
Inspekta Mwagara alidai kuwa hata hivyo katika
ukaguzi wao hawakuweza kupata kielelezo chochote cha kuwasaidia, na
kwamba wakati wakiwa kwa mtuhumiwa huyo, alimtaka mtuhumiwa awaeleze
ukweli kwa kuwa walikuwa wameshachoka
.
.
Alidai kuwa mshtakiwa huyo alisema naye
ameshachoka kuzunguka na kwamba sasa anataka awaeleze ukweli, na ndipo
akasema kuwa Opong tayari wameshamuua, na kwamba yuko tayari kwenda
kuwaonyesha walikomzika.
0 comments:
Post a Comment