Mangula: CCM haitakiwi kutoa maoni
- Akichambua baadhi ya vipengele vya rasimu hiyo, Chikawe alisema haoni kama ni vyema katiba kuruhusu wananchi kumvua ubunge, mbunge ambaye hajatimiza wajibu wake kwani hali hiyo itazua vurugu na fitina.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula
amesema viongozi wa chama hicho hawatakiwi kuichambua rasimu ya katiba
mpya na kutoa maoni binafsi na badala yake wataitembeza rasimu hiyo kwa
wanachama ili waikosoe.
“Unajua sisi ni viongozi na hatutakiwi kutoa maoni
binafsi, sisi tunawawakilisha wananchi ambao ni wanachama wa CCM,
tutawaplekea hao ili watoe maoni yao” alisema Mangula.
Alisema ni vigumu kwa kikao kimoja cha Kamati Kuu
ya CCM kutoa maoni kwa sababu hao ni wawakilishi tu wa chama, hivyo
wanachama wote wa chama hicho watapelekewa rasimu wakaichambue ndipo
chama kitatoa msimamo wake.
“Sisi viongozi hatutoi maoni tutaipeleka rasimu
kwa wanachama wetu zaidi ya 6,000 tuyasikie wanayosema, kwa sababu hao
ndiyo wananchi” alisema Mangula Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias
Chikawe alizungumza na gazeti hili na kusema kuwa ni vyema kama
wananchi ambao CCM inawawakilisha wakatoa maoni kuhusu rasimu hiyo,
ingawa nao viongozi wanaweza kuchangia maoni yao kama wananchi wa
kawaida.
Akichambua baadhi ya vipengele vya rasimu hiyo,
Chikawe alisema haoni kama ni vyema katiba kuruhusu wananchi kumvua
ubunge, mbunge ambaye hajatimiza wajibu wake kwani hali hiyo itazua
vurugu na fitina. Alisema kwa kuwa siasa unafananishwa na mchezo
mchafu, wapinzani wa ndani ya chama wanaweza kufanya fitina na mbunge
aliye