Tuesday, 18 June 2013

CCM yazoa viti vingi vya udiwani

 
Nassari 


  • Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM.


Chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika sehemu mbalimbali ziligubikwa na vurugu wakati hali ilikuwa mbaya zaidi huko Makuyuni mkoani Arusha ambako Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alipigwa na wafuasia wa CCM na kulazimika kulazwa hospitalini.
Pamoja na vurugu hizo, CCM iliendelea kudhihirisha umwamba wake katika ulingo wa siasa baada ya kujizolea viti vingi vya udiwani wakati wa chaguzi ndogo zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini.
Wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa walikuwa wanafuatilia kwa kina chaguzi hizo ili kupima joto la kisiasa nchini.
Uchaguzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Makuyuni wilayani Monduli ambako Mbunge wake ni mwanasiasa maarufu Edward Lowassa.
CCM iliibuka kidedea huko Makuyuni na kufanya maneno ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Lowassa ana misuli ya kuifanya CCM ishinde huko Monduli.
Lowassa alikuwa na kibarua cha kukabiliana na Chadema waliokuwa wanataka kujipenyeza Monduli ambako hawajahi kuwa na kata tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.
Hata hivyo, bado CCM haijapata dawa ya ushindi Pemba kwani kilishindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi wa ubunge wa Chambani.
Chadema kwa upande wake kilitoa changamoto kwa CCM katika chaguzi hizo za kata na hata kujizolea kata mbili za Iyela huko Mbeya na wilayani Hanan’g huko mkoani Manyara.
Nassari apata kichapo Makuyuni
Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM, akiwa katika harakati za uratibu wa shughuli za upigaji kura za udiwani katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli.
Nassari aliyekuwa wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliomshambulia kwa fimbo na
Tukio hilo lilitokea jana kati ya Saa 3:00 na 4:00 katika kituo cha kupigia kura cha Kwa Zaburi wakati mbunge huyo alipofika kuangalia maendeleo ya zoezi la kura

0 comments:

Post a Comment

My Blog List