Ni kilometa 123 kutoka Kilwa Masoko yalipo makao makuu ya Wilaya
ya Kilwa. Katika wilaya hiyo kuna Kijiji cha Makangaga na kuna kivutio
kizuri cha utalii kwa mfano viboko wa ajabu ambao wanatii amri
mbalimbali.
Wakazi wa kijiji hicho chenye wakazi wapatao 1525
wanaotokana na makabila ya Wamwera, Wangindo, Wamakonde, na Wamachinga
ambao wanalitumia eneo hilo kama kivutio cha utalii ambalo linachangia
pato la wakazi wa eneo hilo mpaka taifa kutokana na watalii wa ndani na
nje.
Viboko wa ajabu
Katika Kijiji cha Makangaga, kilometa tisa kutoka
kijijini hapo, kuna Mto Nyange uliosheheni viboko wa ajabu ambao wana
tabia ya ‘kucheka’ na kutii amri zinazotolewa, hakika ukifika unajua
wamefundishwa, ni fursa nzuri ya utalii kama itatumiwa vyema.
Majira ya usiku viboko hao wanapenda kutembea
kando ya maeneo yao kwa ajili ya kujipatia vyakula na sehemu kubwa
wanakula majani na pia wana tabia za ziada.
Zaidi ya miaka 100 iliyopita mto huo uliotengeneza
bwawa na haukuwa na kiboko hata mmoja, wakazi wa maeneo hayo walitumia
bwawa hilo kwa shughuli za uvuvi na mahitaji ya maji kwa kazi za
kawaida.
Mkazi wa eneo hilo Yahaya Selemani Engema anaeleza
chanzo ni mkazi mmoja aliyetajwa kwa jina la Kimombo ambaye alikuwa
mvuvi hodari kwenye bwawa hilo.
Lakini siku moja alipokwenda kuvua hakurejea na historia kuanzia hapo baada ya wananchi kuona kiboko mmoja kwenye bwawa hilo.
“Ndugu zake baada ya kusubiri kwa siku sita
wakiamini atarejea, waliamua kwenda bwawani hapo kwa nia ya kumtafuta,
walimwita kwa kutumia lugha ya kabila la Wamachinga, ajabu baada ya
kutokea Kimombo kama walivyotarajia alitokea kiboko ambaye alicheka kama
ishara ya kuitika, kutokana na hali hiyo ndugu wa familia ya mvuvi huyo
waliamini ndugu yao alizama kwenye bwawa hilo na kubadilika kuwa kiboko
ambao wanatabia ya kucheka,”anasema Omari Yanda mmoja wazee maarufu
kijiini hapo.
Kila mwaka hivi sasa inakadiriwa kuwa wanafikia zaidi ya viboko 300, na kwamba wanatii amri ya ukoo wa Kimombo.
“Familia iliyoshikilia wanyama hao ni ya Kimombo
wanarithishana kwa kuwa kiboko wa kwanza alitoka katika familia hiyo,
wageni wanaofika kuwaona viboko hao huwaita viboko hao kwa kutumia jina
la Kimombo ndipo viboko hao hujitokeza wakicheka,” anasema Yanda.
Miongoni mwa maajabu ya viboko hao ni kuwa wana
uwezo wa kujitokeza pindi wanapohitajika kwa maana wakitakiwa wajitokeze
wadogo wataibuka wadogo na wakitakiwa wajitokeze wazee watajitokeza
wazee wote waliomo bwawani
0 comments:
Post a Comment