Sunday 9 June 2013

Nembo za TRA kusaidia sanaa


Wema Sepetu 0

Dar. Kilio cha muda mrefu cha wasanii wa filamu kuibiwa kazi zao kitaisha baada utaratibu wa kuweka nembo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye mikanda ya filamu kuanza Julai, Mosi, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Maktaba za Video Tanzania, Richard Kalinga alisema hayo Ijumaa iliyopita kwamba kuwekwa kwa nembo hiyo ya TRA itasababisha kazi ya kuwatafuta wanaoiba kazi za wasanii kuwa rahisi.
Alisema hayo kwenye mkutano wa wadau wa filamu ulioandaliwa kwa ajili ya kulinda haki za wasanii wa filamu dhidi ya waharamia na kuifanya sekta hiyo kulipa kodi katika serikali.
Taasisi ya BEST-AC kwa kushirikiana Indigo –MTPC na Media for Development International (MFDI) ndiyo walioitisha mkutano kwa ajili ya kusaidia kuondokana na uharamia wa kazi za wasanii wa filamu.
Kalinga alisema katika utaratibu huo, kazi za filamu zitanunuliwa zikiwa na nembo ya TRA, “mnunuzi akiona mkanda wa filamu anaotaka kuununua hauna nembo hiyo afahamu kwamba huo siyo halisi.
“Mteja akinunua filamu ya aina hiyo afahamu kwamba haitakuwa bora kwa sababu itakuwa imetengenezwa kiholela na kodi ya serikali wanaikwepa,” alisema Kalinga.

0 comments:

Post a Comment

My Blog List