Sunday 9 June 2013

Msanii bongo movie aliyeanza kucheza ulaya


 

Kama utakuwa shabiki na mtazamaji mzuri wa filamu za bongo movie, jina la Lucy Francis Komba halitakuwa jipya masikioni mwako.
Msanii huyu alianza sanaa katika Kundi la Kaole, akishiriki baadhi ya vipindi vya televisheni na baadaye kujiunga na Kikundi cha , Dar Talent ambapo alishiriki filamu moja ya vichekesho
.
Katika sanaa, Lucy ameshacheza filamu zaidi ya 50 zikiwemo nne alizocheza nje ya nchi. Filamu ya kwanza aliyocheza nyota huyu na kuonyesha kipaji chake inafahamika kama Utata. Baadaye alishiriki filamu ya Yolanda, Division of Love, Jeraha la Ndoa, Talaka Wodini, Siri ya Moyo Wangu, Teke la Mama, Richmond, Swadakta na nyinginezo
Kwa sasa Lucy ni mwigizaji wa filamu, mwongozaji, mtunzi wa stori na mtayarishaji wa filamu aliyefanikiwa kuvuka mipaka ya nchi hasa Bongo Movie akichanua hadi katika nchi za Burundi, Sierra Leone na Denmark.
Lucy kwa sasa anasubiri kuzindua filamu yake mpya aliyoichezea nchini Denmark.
”Nilienda kupumzika tu, lakini baada ya kuona wana mwitikio mzuri na filamu zetu, ilinibidi nicheze filamu niliyoipa jina la ‘Tanzania to Denmark’,” anasema Lucy.
Anabainisha kuwa filamu hiyo amecheza kwa gharama zake akishirikiana na Kampuni ya Vad Production ya Denmark inayojihusisha na uzalishaji wa filamu.
“Walinisaidia sana hadi hatua ya mwisho. Natarajia kuizindua mwezi huu wa Juni nchini Denmark, naamini itauza sana, maana nimecheza na wasanii maarufu wa huko,”anasema Lucy.
Aprili mwaka jana, msanii huyo alifanikiwa kwenda nchini Ghana kwa maa
ndalizi ya kucheza filamu yake, hata hivyo hakuweza kufanikiwa baada ya msanii mwenzake Kanumba kufariki dunia.
..........................................................................................................................................................

“Mimi nilikuwa nimeshatangulia, nikiwa huko nikasikia amefariki ikanibidi nirudi kwanza nyumbani kwa mazishi yake,”anasema Lucy.
Kabla ya kuondoka Ghana, Lucy alibahatika kufanya mahojiano na mastaa wa nchini Sierra Leone waliokuwa wakikusanya washiriki wakubwa kwa lengo la kuandaa filamu itakayojitambulisha kimataifa.
Maandalizi hayo ni maarufu kama ‘famous film magazine in Africa’ ambayo imewashirikisha baadhi ya nyota akiwamo Van Vicker, Ini Edo, Desmond na wengineo katika kuandaa filamu ya ‘Repa

0 comments:

Post a Comment

My Blog List