Sunday 9 June 2013


SHARE THIS STORY
0
Share


Dar. Msanii wa muziki wa miondoko ya R’n’B, Benard Paul maarufu kama Ben Pol wiki hii anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa Jikubali ambao ameutoa wiki iliyopita .
Mbali na hilo, Ben Pol ameeleza kuwa siri ya yeye kuingia kwenye vipengele vitano katika tuzo muziki za Kilimanjaro mwaka huu ni kutokana na kazi nzuri anazozifanya ambazo mashabiki wanazikubali na hakuna kingine hivyo alistahili
Aliliambia Mwananchi mwisho wa wiki kuwa mwaka huu umekuwa wenye mafanikio kwake, kwani toka aanze muziki hakutarajia kama ipo siku ataangiza nyimbo kwenye vipengele vingi.
 
 
“Mwaka juzi (2011) niliingiza wimbo mmoja na mwaka jana nyimbo mbili, hapo utaona jinsi gani ninavyopiga hatua kutoka kwenye nyimbo hizo hadi kufikia kuingiza nyimbo tano mwaka huu.
Kwa hakika hili ni jambo la kujivunia , nawashukuru Watanzania kwa msaada wao,” anasema.
Katika hatua nyingine, msanii huyoamewaomba Watanzania wasisite kumpigia kura kwenye kinyang’nyiro hicho ili aweze kunyakuwa tuzo hizo mwaka huu na hatimaye aweke historia ya kuwa msanii wa kwanza wa RnB kunyakua tuzo nyingi.

0 comments:

Post a Comment

My Blog List