Monday 10 June 2013



SASA NINAAMINI NI NUDA MAALUM WA KUIAGA SIASA

 
BIG 4 MILLY


Mwimbaji wa kike aliyewahi kupata umaarufu kupitia wimbo wake , ‘Mr Politician’ Nakaaya Sumari amesema kuwa hatokaa arudie tena kugombea ubunge kwani alikuja kugundua kuwa alikosea kufanya hivyo.
Mwaka 2010 msanii huyo alijaribu kugombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia  chama tawala, CCM lakini alienguliwa kwenye kura za maoni.
Alisema kuwa hataki tena kusikia masuala ya siasa tena kwani baada ya kugombea alijionea vitu vingi ambavyo anaona hataweza kuvifanya hivyo ni vizuri akabaki kuwa msanii.
Baada ya mchakato huo katika Kisiasa na ubunge, msanii huyo alikuwa hasikiki  tena kama ilivyokuwa awali.
Alisema kuwa ukimya huo ulitokana na mambo mbalimbali ya maisha ambapo pia alilazimika kuishi Arusha tofauti na mwanzo ambapo alikuwa akifanya shughuli zake za muziki jijini Dar es Salaam.
Alipokuwa  Arusha Nakaaya alisema alijaribu kuendelea kufanya muziki na pia kujaribu kuwaunganisha wasanii wa  huko kwa kuanzisha chama cha wasanii  mkoani humo ambapo mpaka anarejea Dar es Salaam aliwaacha wakiwa katika hatua ya usajili.
Mwanadada huyo anasema pamoja na hayo ameona kuwa shughuli zake za muziki haziendi kama awali kwasababu akiwa Arusha inakuwa ngumu kusambaza kazi zake.
Kwa sasa, Nakaaya anasema kuwa amerudi Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya muziki wake kwa umakini tena kama awali, na mashabiki wake watarajie vitu vizuri kutoka kwake.
Msanii huyo aliachia wimbo wake mpya,  ‘Utu Uzima’ ambao amemshirikisha Dunga. Wimbo huo umerekodiwa katika studio za FishCrab chini ya Lamar.
Anasema msanii Rich Mavoko pia alimsaidia kuandika wimbo huo.
Msanii huyo  alianza kupata umaarufu kwenye muziki baada ya kushiriki mashindano ya kuimba yanayofanyika Nairobi, Kenya yanayojulikana kama ‘Tusker Project Fame’. Baadaye  alitoa albamu yake kwanza, ‘Nervous Condition’ iliyokuwa na wimbo wa ‘Mr Politician’ uliofanya vizuri  mwaka 2008.

0 comments:

Post a Comment

My Blog List