Tuesday 11 June 2013

Sunday, June 9, 2013

KALA JEREMIAH, OMMY DIMPOZ HATIMAYE WAINUKA KIDEDEA PIA WAFUNIKA KILI MUSIC AWARDS 2013

DAR ES SALAAM, Tanzania HATIMAYE kitendawili cha nani kavuna nini katika kinyang’anyiro Kilimanjaro Tanzania Music Awards KTMA 2013, kilipata jibu usiku wa jana, ambapo kategori 37 za mchakato huo zilipata washindi, huku wasanii Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakifunika kwa upande wa muziki wa kizazi kipya. Kala Jeremiah aliyekuwa karibu atwae tuzo, alijikuta akimaliza kwa kutwaa tuzo tatu za Wimbo Bora wa Mwaka (Dera God), Msanii Bora wa Hip Hop na ile ya Mtunzi Bora Bora wa Hip Hop, huku akiipoteza ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Hip Hop (Dear God) iliyochukuliwa na Nay wa Mitego kuptia wimbo Nasema Nao. Kwa upande wa Dimpoz, nyota pekee aliyekuwa akiwania tuzo saba katika kinyang’anyiro hicho, alipata tuzo tatu za Wimbo Bora wa Bongo Pop (Me and You feat Vanessa Mdee), kibao kilichompa pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano. Dimpoz akapokea tuzo ya tatu ya Video Bora ya Mwaka kupitia kibao cha Baadae, huku akiangukia pua katika kategori nne za Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume – Bongo Flava na Mtunzi Bora wa Mashairi – Bongo Flava. Katika namna iliyowavutia wengi, Dimpoz aliitoa kwa Vanessa Mdee moja ya tuzo mbili alizoshinda kupitia kibao alichomshirikisha cha Me and You kwa, tukio lililotafsiriwa kama ‘kumpoza’ binti huyo aliyeangukia pua katika kategori ya Msanii Bora Anayechipukia, ambayo ilienda kwa Ali Nipishe. Bendi ya Mashujaa waliibuka kidedea zaidi katika mchakato huo, baada ya kujizolea tuzo tano, kupitia mbili za bendi (Wimbo Bora wa Bendi – Risasi Kidole) na Bendi Bora ya Mwaka, huku ikitwaa tatu za wasanii wake, ambao ni Chalz Baba aliyetwaa mbili za Mtunzi Bora wa Mashairi – Bendi na Msanii Bora wa Kiume – Bendi. Pia rapa wake Ferguson aliibuka kidedea katika kategori ya Rappa Bora wa Bendi, alikowabwaga Greyson Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya Radi. Ukiondoa washindi wa Kategori 35, KTMA 2013 ilitoa tuzo mbili maalum; moja ya All of Fame ilitwaliwa na kundi la Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje’ ambayo ilipokelewa na Waziri Ali, huku ile ya Individual All of Fame ikinyakuliwa na nyota wa muziki wa zamani marehemu Salum Abdallah na kupokelewa na mwanaye. Hapa tunakuletea kategori zote 35. Wimbo Bora wa Mwaka; Dear God - Kala Jeremiah Msanii Bora wa Kiume; Diamond Platnumz Msanii Bora wa Kike; Lady Jaydee ‘Comandoo’ Msanii Bora wa Kike wa Taarab; Isha Mashauzi Msanii Bora wa Kiume wa Taarab; Mzee Yusuf Msanii Bora wa Kiume Bongo Flava; Diamond Platnumz Msanii Bora wa Kike Bongo Flava; Recho Msanii Bora wa Hip Hop; Kala Jeremiah Msanii Bora wa Kiume Bendi; Chalz Baba Msanii Bora wa Kike Bendi; Luiza Mbutu Msanii Bora Anayechipukia; Ali Nipishe Video Bora ya Mwaka; Baadae - Ommy Dimpoz Mtunzi Bora wa Taarab; Thabit Abdul Mtunzi Bora wa Bongo Flava; Ben Pol Mtunzi Bora wa Mashairi Hi Hop; Kala Jeremiah Mtunzi Bora wa Mashairi Bendi; Chalz Baba Mtayarishaji Bora wa Mwaka Bongo Flava; Man Water Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka Taarab; Enrico Mtayaraishaji wa Wimbo wa Mwaka Bendi; Amoroso Mtayarisha Bora Anayechipukia; Mensen Selecta Rapa Bora wa Mwaka - Bendi; Fagasoni Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania; Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto Wimbo Bora wa Mwaka - Bendi; Risasi kidole - Mashujaa band Wimbo Bora wa Mwaka - Reggae; Kilimanjaro - Warriors from The East Wimbo Bora wa Afrika Mashariki; Valu Valu - Jose Chameleone Wimbo Bora wa Mwaka Bongo Pop; Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee Wimbo Bora wa Ushirikiano; Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee Wimbo Bora wa Hip Hop; Nasema Nao - Nay wa Mitego Wimbo Bora wa Mwaka wa RnB; Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha Wimbo Bora wa Mwaka wa Ragga/Dancehall; Predator - Dabo Wimbo Bora wa Mwaka wa Taarab; Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa Wimbo Bora wa Mwaka Zouk/Rhumba; Ni wewe - Amini Bendi Bora ya Mwaka; Mashujaa Band Kundi Bora la Mwaka la Taarab; Jahazi Modern Taarab Kundi Bora la Mwaka Bongo Flava; Jambo squadBIG 4 MILL

0 comments:

Post a Comment

My Blog List