Tuesday 11 June 2013

Kagasheki, Lembeli wapingana kwa takwimu

Share bookmark Print Email Rating
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki 
Na Hakimu Mwafongo  (email the author)

Posted  Jumanne,Juni11  2013  saa 21:39 PM
Kwa ufupi
  • Taarifa za Serikali kuwa tembo 10,000 wanauawa kila mwaka si sahihi kwa kuwa zimeandaliwa na maofisa wa Serikali kwa ajili ya kuwatetea.
SHARE THIS STORY
0
Share


Iringa. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, James Lembeli amepinga kauli zilizotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kuhusu tembo wanaouawa nchini kutokana na ujangili.
Waziri Kagasheki alisema kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tawiri, zaidi ya tembo 10,000 huuawa kila mwaka na majangili kitu ambacho kinatishia maisha ya wanyama hao hapa nchini.
Kagasheki alisema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Waandishi wa habari wa Vyombo vya Habari nchini na Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) uliofanyika Iringa jana.
Hata hivyo Lembeli alisema kiasi kilichosemwa na Waziri ni kidogo kwa kuwa watafiti waliotoa takwimu hizi ni wa Serikali hivyo wanaficha baadhi ya mambo.
“Taarifa za Serikali kuwa tembo 10,000 wanauawa kila mwaka si sahihi kwa kuwa zimeandaliwa na maofisa wa Serikali kwa ajili ya kuwatetea,” alisema Lembeli.
Alisema tatizo la ujangili wa meno ya tembo nchini ni kubwa na idadi inayotolewa ni kwa wale tembo wanaouawa kwenye hifadhi tu wakati wengi bado wanauawa na majangili nje ya hifadhi za Taifa.
Aidha aliwataka wanahabari kutokuwa waoga katika kufichua habari za majangili wa meno ya tembo kwa kuwa wanaojihusisha na meno ni watu wenye uwezo mkubwa kifedha na wana mitandao mikubwa.
“Ni vyema wanahabari kutokuwa waoga katika kufichua mitandao ya ujangili kwa kuwa wanaohusika wana fedha na kuna viongozi ambao wanawaunga mkono”, alisema Lembeli.
Akizungumzia umuhimu wa vyombo vya habari Kagasheki alivitaka kuisaidia Serikali kukabiliana na vita dhidi ya ujangili wa tembo na wanyamapori wengine.
Aliwaomba waandishi wa habari kusaidia kwa kuwa kuna rushwa bandarini, viwanja vya ndege, ndani ya Mahakama, serikalini, polisi, idara ya usalama, na mamlaka ya mapato ndiyo maana ujangili hasa wa meno ya tembo unaongezeka.
Alisema watalii havutii kuwaona tembo wanaoendelea kupungua duniani kote kutoka milioni 50 mwaka 1930 hadi 402,067 mwaka jana.
Kagasheki alisema kwa upande wa Tanzania idadi yake imepungua kutoka kati ya tembo 250,000 na 300,000 katika miaka ya sitini hadi hadi 110,000 mwaka 2009

0 comments:

Post a Comment

My Blog List