Tunaishi pamoja wakati wowote
http://www.big4mill.blogspot.com for more info - big4mill.blogspot.com.
Monday, 8 July 2013
QUEEN DARLEEN: KWENYE MAPENZI UBABE NAUWEKA PEMBENI
Thursday, 4 July 2013
FBI wakagua ofisi ya Kova kwa mbwa
. Ofisa mmoja wa Usalama wa Marekani (FBI), akiwa na mbwa jana aliingia Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kufanya ukaguzi.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya msafara
wa magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.
Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi walitoka.
“Walikwenda moja kwa moja mapokezi wakafanya
ukaguzi, kisha wakatoka nje ya jengo na kama hiyo haitoshi, ofisa huyo
akiwa na mbwa alikwenda sehemu ya kuegesha magari yenye kesi na yale ya
kawaida na kuanza kufanya ukaguzi, baada ya hapo waliondoka,” alisema
polisi huyo na kuongeza:
“Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili
la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo
tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”
Hata hivyo, usalama kwenye vituo vingi ikiwamo
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu Nyerere, vilikuwa chini ya
usimamizi na uangalizi wa makachero wa Marekani.
Mandla: Mjukuu anayeinyima usingizi familia ya Mandela
Johannesburg. Mjukuu wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela, Mandla Zwelivelile Mandela ambaye ameibua mgogoro mkubwa katika
familia ya shujaa huyo wa Afrika katika mzozo wa makaburi amekuwa na
mlolongo wa visa katika maisha yake.
Visa hivyo kwa sehemu kubwa vinahusu maisha yake
ya ndoa kwani ameoa na kuacha mara tatu huku akikabiliwa na kisa kingine
cha kudaiwa kuuza haki za televisheni za kuonyesha mazishi ya Mzee
Mandela.
Mandla ambaye jana aliamriwa na Mahakama kurejesha
mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela, alizaliwa mwaka 1974 na
kwa sasa ni Chifu wa eneo la Mvezo. Ni msomi mwenye shahada ya kwanza ya
siasa aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Rhodes mwaka 2007.
Chifu huyo wa Kabila la Xhosa amekuwa na vituko
vingi katika maisha yake. Mwaka 2009 alizua utata baada ya kuuza haki ya
kutangaza mazishi ya Mandela atakapokufa kwenye kituo cha televisheni
cha SABC kwa Rand 3 milioni (Sh481 milioni).
Hata hivyo, suala hilo lilifikishwa katika
Mahakama Kuu ya Mthatha ambako hukumu ilitoka na alipewa siku 15
kutangaza kama kweli ameuza haki ya matangazo ya mazishi ya Mandela au
akanushe taarifa hizo.
Taarifa zilisema kuwa kutokana na shinikizo la
baadhi ya wanafamilia na mkazo wa hukumu ya Mahakama, Mandla alilazimika
kukanusha kuuza haki ya matangazo ya mazishi ya Mandela kwa kituo
kimoja cha televisheni.
Mandla ambaye ni mtoto wa Makgatho Mandela
aliyefariki dunia mwaka 2005 baada ya kuugua maradhi yanayofanana na ya
Ukimwi, alipata hadhi ya uchifu baada ya kifo cha baba yake mwaka 2007.
Mandela ambaye alikabidhiwa uchifu wa uongozi wa
watu wa Kabila la Xhosa takriban miaka 70, ndiye aliyempendekeza Mandla
kuchukua wadhifa huo. Alikabidhiwa wadhifa huo mwaka 2007 wakati huo
akiwa na umri wa miaka 32. Majukumu yake yalikuwa kuongoza sherehe za
kimila, kutatua matatizo ya ndani ya ukoo wao na kuwakilisha Kabila la
Xhosa katika masuala ya kisiasa.
Kutokana na majukumu hayo, Mandla alichaguliwa
kuwa mbunge mwaka 2009 kupitia Chama cha African National Congress
(ANC). Mke wake wa kwanza ni Tando Mabuna-Mandela aliyemuoa mwaka 2004.
Hata hivyo, mwaka 2009, mwanamke huyo aliomba talaka mahakamani akidai
kuwa mumewe huyo ni mgumba.
Mke wa pili wa Mandla ni Anais Grimaud aliyezaliwa
mwaka 1990 huko Reunion ambaye alibadili jina lake na kuitwa Nkosikazi
Nobubele. Walioana Machi 2010 katika ndoa ya kimila.
Septemba 2011 alipata mtoto aliyepewa jina la
Qheya II Zanethemba Mandela na alikaribishwa kwa Mandela kijijini Qunu
kwa taratibu za kimila. Hata hivyo, Agosti mwaka 2012, Mandla alimkataa
mtoto huyo akidai mkewe alikuwa ana uhusiano na kaka yake, kesi ilifika
mahakamani na waliachana kutokana na sababu hiyo.
Mkewe wa tatu ni Nodiyala Mbali Makhathini ambaye walioana Desemba 24, 2011, lakini tayari amefungua kesi ya kudai talaka.
Michelle Obama: Acheni kufuatilia mavazi yangu
Dar es Salaam. Michelle Obama na Laura Bush
walikuwa kivutio jana kwenye Mkutano wa wake wa marais wa Afrika
unaoendelea Dar es Salaam, pale walipoongelea kwa mzaha jinsi vyombo vya
habari vinavyoshupalia kuandika kuhusu staili za nywele na mavazi ya
wake wa marais, huku vikiacha masuala ya msingi.
Mkutano huo uliofunguliwa jana na Rais Jakaya
Kikwete, ni maalumu kwa ajili ya kusaidia wanawake wajasiriamali wa
Afrika, unatarajiwa kumalizika leo
.
.
Wakizungumza kwenye mjadala ulioongozwa na
Mwandishi wa Habari wa Marerkani, Cokie Roberts, Michelle, ambaye ni
mke wa Rais wa Marekani, Barack Obama, alisema alifurahia kupata nafasi
ya kufanya majadiliano na Laura, ambaye ni mke wa Rais wa zamani wa
Marekani.
“Ninampenda mwanamke huyu,” alisema Michelle kwa utani kama vile hamfahamu.
“Sishangai sana maana tuko klabu moja nadhani,”
alijibu Laura kwa utani akiwa na maana kuwa, wao wote wana uzoefu wa
kuwa wake wa marais.
“Unajua tunaishi maisha ya shida, maana wenzetu wa
habari wanaangalia zaidi staili za mavazi na nywele zetu badala ya
kuangalia mambo ya msingi,” alisema Michelle.
Alisema mwanzoni mwa mwaka huu, alibadili staili
ya nywele lakini alishangaa jinsi suala hilo lilivyokuzwa na vyombo vya
habari.
Pinda aisaliti kauli yake, aruhusu tena sherehe
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewaagiza
Watanzania kuwa na uzalendo wa kuwaenzi na kuwakumbuka wenzao ambao
wamefanya kazi muda mrefu kwa kuthamini mchango wao.
Pinda alitoa kauli hiyo juzi katika viwanja vya
Bunge, aliposhiriki hafla ya kuwaaga wafanyakazi waliostaafu utumishi na
wale waliohamishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuanzia 2010.
Hata hivyo, Pinda alisema yeye ndiye aliyemwagiza
Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia kuandaa hafla hiyo ili kuwatunuku
zawadi na kula nao chakula pamoja na watumishi hao, ambao idadi yao
ilikuwa 59 kutoka sehemu mbalimbali nchini. Hata hivyo walihudhuria 35.
Juzi ilikuwa ni siku ya pili mfululizo kwa Pinda
kushirikia warsha katika viwanja hivyo, siku iliyotangulia alikuwa
ameshiriki sherehe kubwa iliyoandaliwa na Bunge kumwaga Spika Mstaafu
ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
ambaye alitumikia nafasi ya Uspika kwa miaka mitano 2005/10.
Sherehe ya juzi ambayo iliandaliwa kwa agizo la
Pinda, inapingana na kauli na maagizo yake ambayo amekuwa akitoa kwa
nyakati tofauti kwamba, makongamano na warsha zisizo na tija ni ufujaji
fedha za umma.
“Mimi ndiye niliyeamua kufanya hivi na huu ni
ubinadamu tu nikaona nimtume mama Ghasia afanye maandalizi hayo, lengo
kuu la hapa ni kukaa pamoja na wenzetu na kuwaambia kuwa tunashukuru kwa
kazi yenu nzuri na pia tunathamini michango yenu,” alisema Pinda.
Alisema huo ulikuwa ni mwanzo, lakini Tamisemi
itakuwa ikifanya hivyo kila mwaka kuwaaga watu wanaostaafu na
wanaohamia wizara zingine.
Kuhusu wastaafu hao, alisema Serikali inapaswa
kuwathamini na kutambua michango yao wakati wote kuliko kuwatelekeza
kama ilivyo sasa.
Alisema kustaafu kwa mtu sio kwamba anakuwa
amepungukiwa hekima na maarifa, bali ni utaratibu ukifika wakati fulani
anatakiwa kupumzika.
Licha ya hilo, aliwaagiza viongozi wa Tamisemi
kuangalia uwezekano wa kuwasaidia watu wanaojiandaa kustaafu ili wajenge
nyumba za kufikia na familia zao, kwani wengine humaliza muda na
kushindwa kujenga.
Tangu kuingia ateuliwe, Pinda amekuwa akipiga vita
sherehe na ununuzi wa magari ya kifahari kwa madai kuwa, ni ubadhirifu
wa fedha za umma.
Hatua hiyo inaonyesha ameanza kubariki fedha hizo kufanya sherehe.









