“Watu wanapaswa kuelewa, wake za marais nao hufanya mambo mazuri ya
jamii na kazi yao siyo kubadili staili za nywele na mavazi tu,”
Michelle Obama
Dar es Salaam. Michelle Obama na Laura Bush
walikuwa kivutio jana kwenye Mkutano wa wake wa marais wa Afrika
unaoendelea Dar es Salaam, pale walipoongelea kwa mzaha jinsi vyombo vya
habari vinavyoshupalia kuandika kuhusu staili za nywele na mavazi ya
wake wa marais, huku vikiacha masuala ya msingi.
Mkutano huo uliofunguliwa jana na Rais Jakaya
Kikwete, ni maalumu kwa ajili ya kusaidia wanawake wajasiriamali wa
Afrika, unatarajiwa kumalizika leo
.
.
Wakizungumza kwenye mjadala ulioongozwa na
Mwandishi wa Habari wa Marerkani, Cokie Roberts, Michelle, ambaye ni
mke wa Rais wa Marekani, Barack Obama, alisema alifurahia kupata nafasi
ya kufanya majadiliano na Laura, ambaye ni mke wa Rais wa zamani wa
Marekani.
“Ninampenda mwanamke huyu,” alisema Michelle kwa utani kama vile hamfahamu.
“Sishangai sana maana tuko klabu moja nadhani,”
alijibu Laura kwa utani akiwa na maana kuwa, wao wote wana uzoefu wa
kuwa wake wa marais.
“Unajua tunaishi maisha ya shida, maana wenzetu wa
habari wanaangalia zaidi staili za mavazi na nywele zetu badala ya
kuangalia mambo ya msingi,” alisema Michelle.
Alisema mwanzoni mwa mwaka huu, alibadili staili
ya nywele lakini alishangaa jinsi suala hilo lilivyokuzwa na vyombo vya
habari.
0 comments:
Post a Comment