SASA NINAAMINI NI NUDA MAALUM WA KUIAGA SIASA
BIG 4 MILLY
Mwimbaji wa kike aliyewahi kupata umaarufu
kupitia wimbo wake , ‘Mr Politician’ Nakaaya Sumari amesema kuwa hatokaa
arudie tena kugombea ubunge kwani alikuja kugundua kuwa alikosea
kufanya hivyo.
Mwaka 2010 msanii huyo alijaribu kugombea ubunge
wa Arusha Mjini kupitia chama tawala, CCM lakini alienguliwa kwenye
kura za maoni.
Alisema kuwa hataki tena kusikia masuala ya siasa tena kwani baada ya kugombea alijionea vitu vingi ambavyo anaona hataweza kuvifanya hivyo ni vizuri akabaki kuwa msanii.
Alisema kuwa hataki tena kusikia masuala ya siasa tena kwani baada ya kugombea alijionea vitu vingi ambavyo anaona hataweza kuvifanya hivyo ni vizuri akabaki kuwa msanii.
Baada ya mchakato huo katika Kisiasa na ubunge, msanii huyo alikuwa hasikiki tena kama ilivyokuwa awali.
Alisema kuwa ukimya huo ulitokana na mambo
mbalimbali ya maisha ambapo pia alilazimika kuishi Arusha tofauti na
mwanzo ambapo alikuwa akifanya shughuli zake za muziki jijini Dar es
Salaam.
Alipokuwa Arusha Nakaaya alisema alijaribu
kuendelea kufanya muziki na pia kujaribu kuwaunganisha wasanii wa huko
kwa kuanzisha chama cha wasanii mkoani humo ambapo mpaka anarejea Dar
es Salaam aliwaacha wakiwa katika hatua ya usajili.
Mwanadada huyo anasema pamoja na hayo ameona kuwa
shughuli zake za muziki haziendi kama awali kwasababu akiwa Arusha
inakuwa ngumu kusambaza kazi zake.
Kwa sasa, Nakaaya anasema kuwa amerudi Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya muziki wake kwa umakini tena kama awali, na mashabiki wake watarajie vitu vizuri kutoka kwake.
Kwa sasa, Nakaaya anasema kuwa amerudi Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya muziki wake kwa umakini tena kama awali, na mashabiki wake watarajie vitu vizuri kutoka kwake.
Msanii huyo aliachia wimbo wake mpya, ‘Utu Uzima’
ambao amemshirikisha Dunga. Wimbo huo umerekodiwa katika studio za
FishCrab chini ya Lamar.
Anasema msanii Rich Mavoko pia alimsaidia kuandika wimbo huo.
Anasema msanii Rich Mavoko pia alimsaidia kuandika wimbo huo.
Msanii huyo alianza kupata umaarufu kwenye muziki
baada ya kushiriki mashindano ya kuimba yanayofanyika Nairobi, Kenya
yanayojulikana kama ‘Tusker Project Fame’. Baadaye alitoa albamu yake
kwanza, ‘Nervous Condition’ iliyokuwa na wimbo wa ‘Mr Politician’
uliofanya vizuri mwaka 2008.
0 comments:
Post a Comment