KALA JEREMIAH, OMMY DIMPOZ HATIMAYE WAINUKA KIDEDEA PIA WAFUNIKA KILI MUSIC AWARDS 2013
DAR ES SALAAM, Tanzania
HATIMAYE kitendawili cha nani kavuna nini katika kinyang’anyiro
Kilimanjaro Tanzania Music Awards KTMA 2013, kilipata jibu usiku wa
jana, ambapo kategori 37 za mchakato huo zilipata washindi, huku wasanii
Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakifunika kwa upande wa muziki wa kizazi
kipya.
Kala Jeremiah aliyekuwa karibu atwae tuzo, alijikuta akimaliza kwa
kutwaa tuzo tatu za Wimbo Bora wa Mwaka (Dera God), Msanii Bora wa Hip
Hop na ile ya Mtunzi Bora Bora wa Hip Hop, huku akiipoteza ya Wimbo Bora
wa Mwaka wa Hip Hop (Dear God) iliyochukuliwa na Nay wa Mitego kuptia
wimbo Nasema Nao.
Kwa upande wa Dimpoz, nyota pekee aliyekuwa akiwania tuzo saba katika
kinyang’anyiro hicho, alipata tuzo tatu za Wimbo Bora wa Bongo Pop (Me
and You feat Vanessa Mdee), kibao kilichompa pia tuzo ya Wimbo Bora wa
Ushirikiano.
Dimpoz akapokea tuzo ya tatu ya Video Bora ya Mwaka kupitia kibao cha
Baadae, huku akiangukia pua katika kategori nne za Wimbo Bora wa Mwaka,
Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume – Bongo
Flava na Mtunzi Bora wa Mashairi – Bongo Flava.
Katika namna iliyowavutia wengi, Dimpoz aliitoa kwa Vanessa Mdee moja ya
tuzo mbili alizoshinda kupitia kibao alichomshirikisha cha Me and You
kwa, tukio lililotafsiriwa kama ‘kumpoza’ binti huyo aliyeangukia pua
katika kategori ya Msanii Bora Anayechipukia, ambayo ilienda kwa Ali
Nipishe.
Bendi ya Mashujaa waliibuka kidedea zaidi katika mchakato huo, baada ya
kujizolea tuzo tano, kupitia mbili za bendi (Wimbo Bora wa Bendi –
Risasi Kidole) na Bendi Bora ya Mwaka, huku ikitwaa tatu za wasanii
wake, ambao ni Chalz Baba aliyetwaa mbili za Mtunzi Bora wa Mashairi –
Bendi na Msanii Bora wa Kiume – Bendi.
Pia rapa wake Ferguson aliibuka kidedea katika kategori ya Rappa Bora wa
Bendi, alikowabwaga Greyson Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya
Radi.
Ukiondoa washindi wa Kategori 35, KTMA 2013 ilitoa tuzo mbili maalum;
moja ya All of Fame ilitwaliwa na kundi la Kilimanjaro Band ‘Wana
Njenje’ ambayo ilipokelewa na Waziri Ali, huku ile ya Individual All of
Fame ikinyakuliwa na nyota wa muziki wa zamani marehemu Salum Abdallah
na kupokelewa na mwanaye.
Hapa tunakuletea kategori zote 35.
Wimbo Bora wa Mwaka; Dear God - Kala Jeremiah
Msanii Bora wa Kiume; Diamond Platnumz
Msanii Bora wa Kike; Lady Jaydee ‘Comandoo’
Msanii Bora wa Kike wa Taarab; Isha Mashauzi
Msanii Bora wa Kiume wa Taarab; Mzee Yusuf
Msanii Bora wa Kiume Bongo Flava; Diamond Platnumz
Msanii Bora wa Kike Bongo Flava; Recho
Msanii Bora wa Hip Hop; Kala Jeremiah
Msanii Bora wa Kiume Bendi; Chalz Baba
Msanii Bora wa Kike Bendi; Luiza Mbutu
Msanii Bora Anayechipukia; Ali Nipishe
Video Bora ya Mwaka; Baadae - Ommy Dimpoz
Mtunzi Bora wa Taarab; Thabit Abdul
Mtunzi Bora wa Bongo Flava; Ben Pol
Mtunzi Bora wa Mashairi Hi Hop; Kala Jeremiah
Mtunzi Bora wa Mashairi Bendi; Chalz Baba
Mtayarishaji Bora wa Mwaka Bongo Flava; Man Water
Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka Taarab; Enrico
Mtayaraishaji wa Wimbo wa Mwaka Bendi; Amoroso
Mtayarisha Bora Anayechipukia; Mensen Selecta
Rapa Bora wa Mwaka - Bendi; Fagasoni
Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania; Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat
Ditto
Wimbo Bora wa Mwaka - Bendi; Risasi kidole - Mashujaa band
Wimbo Bora wa Mwaka - Reggae; Kilimanjaro - Warriors from The East
Wimbo Bora wa Afrika Mashariki; Valu Valu - Jose Chameleone
Wimbo Bora wa Mwaka Bongo Pop; Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa
Mdee
Wimbo Bora wa Ushirikiano; Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Wimbo Bora wa Hip Hop; Nasema Nao - Nay wa Mitego
Wimbo Bora wa Mwaka wa RnB; Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha
Wimbo Bora wa Mwaka wa Ragga/Dancehall; Predator - Dabo
Wimbo Bora wa Mwaka wa Taarab; Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa
Wimbo Bora wa Mwaka Zouk/Rhumba; Ni wewe - Amini
Bendi Bora ya Mwaka; Mashujaa Band
Kundi Bora la Mwaka la Taarab; Jahazi Modern Taarab
Kundi Bora la Mwaka Bongo Flava; Jambo squad
BIG 4 MILL
Posted in:
0 comments:
Post a Comment